MADAKTARI BINGWA WA HOSPITALI YA RUFAA MWANANYAMALA WASHIRIKI KAMBI YA MABINGWA WA RAIS SAMIA LIGULA - MTWARA.
Posted on: May 6th, 2025
Madktari Bingwa zaidi ya sita (06) na wataalamu wa dawa za usingizi kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala, ni miongoni mwa mabingwa wanaoshiriki katika kambi ya madaktari bingwa na mabingwa bobezi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inayoendelea kufanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Ligula-Mtwara.
Madaktari hao ni mabingwa waliobobea katika magonjwa ya Akina Mama, Kinywa na Meno, Macho, Magonjwa ya Ndani, Mionzi, pamoja na mtaalamu wa dawa za usingizi.
Kambi hiyo imeanza tangu Mei 05, 2025 na inatarajiwa kukamilika Mei 09, 2025.
Kambi hiyo ya madaktari Bingwa Kanda ya kusini Mashariki inahusisha Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi kutoka Hospitali za Rufaa za Mkoa Ligula , Mwananyamala, Amana, Temeke, Sokoine-Lindi na Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini, imezinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Abdalah Mwaipaya ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa huo.