Ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto washika kasi

Posted on: September 28th, 2019

Katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora na uboreshaji wa majengo ya kutosha kwa wagonjwa, jengo la mama na mtoto linajengwa kwa kasi ya ajabu ambapo mafundi wameonekana kufanya kazi usiku na mchana. Ujenzi huo ulianza mwaka 2018 lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa taasisi ulisimama kwa muda. La kushangaza ujenzi huo umeanza kwa mafundi kufanya kazi usiku na mchana na kuifanya jamii inayozunguka maeneo hayo kupata taharuki na kujisemea kweli ni kasi ya awamu ya tano.