Kliniki ya Ngozi
Posted on: February 10th, 2026Kliniki ya Ngozi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala hutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa mbalimbali ya ngozi kwa wagonjwa wa huduma za umma (Public), bima na binafsi (Private). Huduma hutolewa kulingana na ratiba ifuatayo:
Jumatatu na Jumatano huduma hutolewa kwa Public, Bima na Private kuanzia saa 7:30 asubuhi hadi 1:30 jioni;
Jumanne huduma hutolewa kwa Private na Bima kuanzia saa 9:00 asubuhi hadi 1:30 jioni;
Alhamisi na Ijumaa huduma hutolewa kwa Private na Bima kuanzia saa 9:00 asubuhi hadi 3:30 jioni.



