Kliniki ya Kisukari

Posted on: January 28th, 2026

Huduma za matibabu ya Kisukari
Kliniki ya Kisukari hutoa huduma za uchunguzi, matibabu na ufuatiliaji wa wagonjwa wa kisukari kwa watu wazima na watoto. Jumatatu, Jumatano na Ijumaa ni siku za ufuatiliaji wa wagonjwa watu wazima na utoaji wa dawa; Jumanne ni kwa wagonjwa wapya pamoja na elimu ya afya; na Alhamisi ni kliniki maalum ya kisukari kwa watoto.