Ukaribisho

profile

Dr. Aileen K. Barongo
Kaimu Mganga Mfawidhi


Karibu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala.

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala ni hospitali ya umma inayotoa huduma za rufaa za kibingwa na kibobezi kwa wakazi takribani milioni 2.2 wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na maeneo ya viunga vya jirani, hususan wilaya za Kinondoni na Ubungo. Hospitali hii ina jukumu muhimu katika utoaji wa huduma za afya za kiwango cha juu, ikiwa ni pamoja na matibabu ya dharura, uchunguzi, tiba na ufuatiliaji wa wagonjwa wa rufaa.

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala inaongozwa na maono ya kuwa hospitali inayoongoza kitaifa katika utoaji wa huduma za afya za rufaa zenye ubora uliotukuka, kwa kuzingatia weledi wa kitaaluma, matumizi ya teknolojia ya kisasa, na utoaji wa huduma zenye huruma, usawa na ufanisi kwa jamii.