BODI YA USHAURI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA MWANANYAMALA YAZINDULIWA RASMI.
Posted on: August 19th, 2025
Uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala yenye wajumbe mbalimbali umefanyika Agosti 15, 2025, bodi hiyo inatarajiwa kutoa ushauri wa kitaalam na kusaidia menejimenti ya hospitali katika kupanga na kusimamia utekelezaji wa mikakati ya kuboresha huduma kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mgeni rasmi Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Bi. Warda Obathany, ameitaka bodi kushirikiana kwa karibu na menejimenti ya hospitali na wadau wa afya mbalimbali ili kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakidhi viwango bora vinavyotarajiwa.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Mohamed Mang’una, amesema ofisi yake itashirikiana kikamilifu na bodi hiyo ili kuhakikisha majukumu yake yanatekelezwa ipasavyo, huku Mwakilishi wa Wizara ya Afya, Dkt. Fadhili Kibaya, akisema kuwa wizara itaendelea kushirikiana na hospitali na uongozi wake kwa lengo la kutimiza azma ya serikali ya kutoa huduma bora na za kisasa kwa wananchi wote.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya hosptali hiyo, Bw. Erasto Mfugale, amesema miongoni mwa vipaumbele vyao ni kutekeleza sera na maelekezo ya Wizara ya Afya ili kuboresha utolewaji wa huduma za afya hospitalini hapo.
Naye Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala, Dkt. Aileen Barongo, amesema bodi ya ushauri ni chombo muhimu kinachosaidia kushauri na kusimamia utekelezaji wa mikakati ya maendeleo ya hospitali, kuboresha matumizi ya rasilimali na kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma bora kwa wakati.
Bodi ya ushauri katika hospitali za rufaa ina wajibu wa kutoa ushauri wa kitaalam kwa menejimenti, kufuatilia ubora wa huduma, kushauri kuhusu matumizi bora ya rasilimali, na kusaidia kuunganisha maoni ya wadau mbalimbali ikiwemo serikali, jamii na wahisani. Hatua ya kuanzishwa kwa bodi hii katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala inatarajiwa kuongeza ufanisi na uwajibikaji, sambamba na mkakati wa kitaifa wa kuboresha huduma za afya nchini.