Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala Waendesha Zoezi la Uchangiaji Damu Kigogo Dar es Salaam.

Posted on: August 10th, 2023


Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala kwa kushirikiana na Taasisi ya JAI Tanzania katika kuadhimisha Wiki ya JAI Kitaifa wamehamasisha na kuendesha zoezi la uchangiaji damu katika Msikiti wa Kigogo 'Round About'  na Msikiti wa 'Masjid Islah' ambapo Kupitia zoezi hilo jumla ya chupa 48 za damu zimekusanywa.

Zoezi hili  litahitimishwa siku ya tarehe 13.8.2023 katika Hospitali ya  Rufaa ya Mkoa Mwananyamala ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya Wiki ya JAI Kitaifa. 

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala inawakaribisha wananchi wote  kujitokeza kwa wingi  kuchangia damu katika siku hiyo. Changia Damu Okoa Maisha. @changiadamutz @wizara_afyatz