MWANANYAMALA RRH YANG'ARA KWA USHINDI KATIKA BONANZA LA MICHEZO YA CHUO CHA USTAWI WA JAMII

Posted on: December 5th, 2023

MWANANYAMALA RRH YANG'ARA KWA USHINDI  KATIKA BONANZA LA MICHEZO YA CHUO CHA USTAWI WA JAMII

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala leo imekuwa kivutio kikubwa kwa kuibuka na ushindi katika michezo mbalimbali ya jadi iliyochezwa katika bonanza la michezo lililoandaliwa na chuo cha Ustawi wa Jamii na kushirikisha timu kutoka katika taasisi mbalimbali  ikiwa ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho.

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala imekuwa ni taasisi pekee iliyotoa washindi wengi katika michezo hiyo ya jadii ambapo wachezaji walioibuka na ushindi walishiriki katika michezo mbalimbali kama vile kuvuta kamba, riadha, mchezo wa bao, karata, mbio za  magunia pamoja na mchezo wa pool table na kukimbiza kuku hivyo kupelekea kukusanya jumla ya medali 12 zilitokana na ushindi katika michezo hiyo.