WAUGUZI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA MWANANYAMALA WAADHIMISHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI, WASISITIZWA UTOAJI WA HUDUMA BORA.

Posted on: May 29th, 2025

Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa Mwananyamala mapema Mei 28, 2025 wameadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani kwa kufanya hafla fupi iliyolenga kujikumbusha dhamana ya kazi yao katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Katika tukio hilo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mwananyamala Dkt. Zavery Benela amewapongeza wauguzi kwa moyo wao wa kujituma na ubunifu katika kuhudumia wagonjwa huku akiwasisitiza kuendelea kufanya kazi kwa moyo.


Kwa upande wake Muuguzi mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Sr. Bertha Mathia, amewataka wauguzi kuendelea kufanya kazi kwa weledi, huruma na uadilifu, akisema kuwa jamii inawategemea kwa kiwango kikubwa.


Katika hatua nyingine, Wauguzi wametumia nafasi hiyo kukata keki maalumu iliyoandaliwa kama sehemu ya kuadhimisha siku hiyo na kutafakari jinsi ya kuimarisha huduma wanazotoa kila siku kwa wagonjwa wanaowahudumia.