Wizara ya Afya yapanga mikakati ya Magonjwa yasiyo ambukizi

Posted on: September 29th, 2019

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoo Dr. Zainab Chaula ameanza kupanga mikakati ya uzinduzi wa kampeni ya magonjwa yasiyo ambukizi. Mikakati hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Protea septemba 17 hadi 18 mwaka huu ambapo aliipanga timu yake vizuri kikazi. Katika tukio hilo Dr. Chaula aliwasisitiza wataalam wake na kuwataka wakafanye kazi kwa weledi kwa kufuata sheria, taratibu na miongozo ya utumishi wa umma.