Saratani ya Matiti

Posted on: February 23rd, 2020

SARATANI YA MATITI


Saratani ya matiti ni uvimbe katika titi usiokuwa na maumivu. Mwanamke yeyote anaweza kuwa nao biia yeye mwenyewe kujua. Ni muhimu kila mwanamke kufahamu jinsi ya kujichunguza mwenyewe ili kugundua mapema kama anao ugonjwa.


Dalili za Saratani ya Matiti

  • Kivimbe katika titi au kwapani kisichokua na maumivu
  • Mabadiliko katika umbo au ukubwa wa titi 
  • Mabadiliko katika umbo Ia ngozi ya titi (kuwa kama ganda la chungwa) 
  • Kutokwa na majimaji machafu au damu katika chuchu 
  • Mabadiliko katika chuchu, kama vile chuchu kuvutwa ndani ya titi


Uchunguzi wa saratani ya matiti

Ni vyema wanawake kuanza uchunguzi wa matiti mapema kuanzia umri wa miaka 18 na kuendelea. Uchunguzi ufanyike mara moja kila mwezi, kati ya siku 3-5 baada ya kumaliza hedhi. Mwanamke aliyesitisha/ aliyekoma hedhi anaweza kujichunguza mwenyewe tarehe moja kila mwezi. Vipimo vya kitaalamu hushauriwa punde tu tatizo linapogunduliwa.


Kumbuka

  • 9 kati ya kila vivimbe 10 kwenye matiti ni magojwa yasiyo saratani 
  • Saratani ya matiti haiambukizi 
  • Asilimia moja ya wanaume hupata saratani ya matiti 
  • Mionzi hutumika kwenye tiba ya saratani ya matiti na sio chanzo cha saratani hiyo 
  • Kuondoa titi mapema ni tiba mojawapo ya saratani ya matiti na sio sababu ya kifo


Kujilinda mapema

  • Kuwa na uzoefu wa kujichunguza mwenyewe matiti yako mara kwa mara 
  • Kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu angalau mara moja kwa mwaka  Kufanyiwa uchunguzi wa matiii kwa njia ya mionzi angalau mara moja kwa mwaka kwa wenye umri zaidi ya miaka 40 
  • Kupunguza/kuacha matumizi ya sigara na tumbaku 
  • Kupunguza/kuacha matumizi ya mafuta kwa wingi kwenve chakula hasa yale yatokanayo na wanyama 
  • Kula mbogamboga na matunda mara kwa mara  Kuwa na uzito usiozidi 
  • Kunyonyesha mtoto kwa muda mrefu iwezekanavyo