Saratani ya Mapafu
Posted on: February 23rd, 2020SARATANI YA MAPAFU
Mambo yanayoongeza uwezekano wa kupata saratani ya mapafu
- Uvutaji wa moshi wa sigara au tumbaku
- Uvutaji wa hewa zenye kemikali za sumu kutoka viwandani
Dalili zinazowezesha kujitokeza
- Kukohoa kwa muda mrefu hata baada ya kutumia dawa
- Kukosa hamu ya kula
- Kukosa pumzi
- Maumivu ya kifua
- Kukonda
Hatua za kuchukua ili kujikinga na saratani ya mapafu
- Epuka kuvuta sigara
- Epuka kukaa karibu na wavuta sigara
- Ishi katika mazingira yenye hewa safi na salama