Public Health Education

SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Ni nini chanzo chake

Saratani ya shingo ya kizazi husababishwa na aina ya kirusi kinachoitwa Human Papilloma (HPV). Kirusi hiki huambukizwa kwa njia ya kujamiiana na mtu mwenye maambukuzi ya HPV


Dalili zake

  • Kutokwa na majimaji au uchafu kusiko kwa kawaida ukeni  Kutokwa na damu kidogo au nyingi ukeni wakati wa kujamiiana 
  • Kutokwa na damu kidogo au nyingi ukeni wakati ambao mwanamke hayuko kwenye hedhi. 
  • Maumivu wakati wa kujamiiana 
  • Kutokwa na damu ukeni kwa wanawake waliokwisha koma hedhi  Maumivu sehemu ya nyonga au chini ya tumbo


Tabia hatarishi zinazochangia saratani ya shingo ya kizazi

  • Kuanza ngono mapema katika umri mdogo (chini ya miaka 18) 
  • Uvutaji wa sigara au tumbaku 
  • Kuwa na wapenzi wengi au kujamiiana na mtu mwenye wapenzi wengi 
  • Matumizi ya mafuta mengi kwenye chakula au kula vyakula vyenye mafuta kwa wingi hasa yale yatokanayo na wanyama 
  • Kutokula mboga za majani na matunda mara kwa mara 
  • Kuzaa idadi kubwa ya watoto hasa wanawake walioanza kuzaa wakiwa na umri mdogo (chini ya miaka 18)


Uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi?

Kwa kufanyiwa uchunguzi wa shingo ya kizazi na wataalamu wa afya angalau mara 1 kwa mwaka


Kuepuka uwezekano wa kupata saratani ya shingo ya kizazi

  • Kuepuka ngono katika umri mdogo, chini ya miaka 18 
  • Kuwa na mwenzi mmoja mwaminifu  Kutumia kondomu wakati wa kujamiiana 
  • Kuepuka uvutaji wa sigara na tumbaku  Kula matunda na mboga za majani kwa wingi 
  • Kuepuka matumizi ya mafuta mengi kwenye chakula hasa yale yatokanayo na wanyama 
  • Kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi angalau mara 1 kwa mwaka 
  • Kuwahi mapema kwa uchunguzi na matibabu punde tu upatapo dalili
read more
SARATANI YA MATITI

SARATANI YA MATITI


Saratani ya matiti ni uvimbe katika titi usiokuwa na maumivu. Mwanamke yeyote anaweza kuwa nao biia yeye mwenyewe kujua. Ni muhimu kila mwanamke kufahamu jinsi ya kujichunguza mwenyewe ili kugundua mapema kama anao ugonjwa.


Dalili za Saratani ya Matiti

  • Kivimbe katika titi au kwapani kisichokua na maumivu
  • Mabadiliko katika umbo au ukubwa wa titi 
  • Mabadiliko katika umbo Ia ngozi ya titi (kuwa kama ganda la chungwa) 
  • Kutokwa na majimaji machafu au damu katika chuchu 
  • Mabadiliko katika chuchu, kama vile chuchu kuvutwa ndani ya titi


Uchunguzi wa saratani ya matiti

Ni vyema wanawake kuanza uchunguzi wa matiti mapema kuanzia umri wa miaka 18 na kuendelea. Uchunguzi ufanyike mara moja kila mwezi, kati ya siku 3-5 baada ya kumaliza hedhi. Mwanamke aliyesitisha/ aliyekoma hedhi anaweza kujichunguza mwenyewe tarehe moja kila mwezi. Vipimo vya kitaalamu hushauriwa punde tu tatizo linapogunduliwa.


Kumbuka

  • 9 kati ya kila vivimbe 10 kwenye matiti ni magojwa yasiyo saratani 
  • Saratani ya matiti haiambukizi 
  • Asilimia moja ya wanaume hupata saratani ya matiti 
  • Mionzi hutumika kwenye tiba ya saratani ya matiti na sio chanzo cha saratani hiyo 
  • Kuondoa titi mapema ni tiba mojawapo ya saratani ya matiti na sio sababu ya kifo


Kujilinda mapema

  • Kuwa na uzoefu wa kujichunguza mwenyewe matiti yako mara kwa mara 
  • Kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu angalau mara moja kwa mwaka  Kufanyiwa uchunguzi wa matiii kwa njia ya mionzi angalau mara moja kwa mwaka kwa wenye umri zaidi ya miaka 40 
  • Kupunguza/kuacha matumizi ya sigara na tumbaku 
  • Kupunguza/kuacha matumizi ya mafuta kwa wingi kwenve chakula hasa yale yatokanayo na wanyama 
  • Kula mbogamboga na matunda mara kwa mara  Kuwa na uzito usiozidi 
  • Kunyonyesha mtoto kwa muda mrefu iwezekanavyo


read more
SARATANI YA NGOZI

SARATANI YA NGOZI

Saratani ya ngozi zipo za aina nyingi. Katika  mada hii saratani ya kaposis saicoma imejadiliwa. Imejadiliwa. Mambo yanayoongeza uwezekano wa kupata saratani hii ni;

  • Kuwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI
  • Upungufu wa kinga mwilini

 

Dalili zinazoweza kujitokeza

  • Mapele meusi na magumu yasiyouma kwenye ngozi
  • Kuvimba miguu na ngozi kuwa ngumu


Kujikinga na saratani ya ngozi

  • Epuka ngono zembe
  • Kufuata ulaji na mtindo bora wa maisha


read more
SARATANI YA MAPAFU

SARATANI YA MAPAFU

Mambo yanayoongeza uwezekano wa kupata saratani ya mapafu

  • Uvutaji wa moshi wa sigara au tumbaku
  • Uvutaji wa hewa zenye kemikali za sumu kutoka viwandani

Dalili zinazowezesha kujitokeza

  • Kukohoa kwa muda mrefu hata baada ya kutumia dawa
  • Kukosa hamu ya kula
  • Kukosa pumzi
  • Maumivu ya kifua
  • Kukonda

Hatua za kuchukua ili kujikinga na saratani ya mapafu

  • Epuka kuvuta sigara
  • Epuka kukaa karibu na wavuta sigara
  • Ishi katika mazingira yenye hewa safi na salama

 

read more
SARATANI

Magonjwa ya Saratani

Saratani hutokea wakati sehemu ya mwili inapokua na kuongezeka bila utaratibu na kusababisha uvimbe. Kwa kawaida saratani huanza taratibu na huchukua muda kuonyesha dalili zozote. Pia dalili za awali haziambatani na maumivu hivyo kusababisha wagonjwa wengi kuchelewa kutafuta matibabu. 


Kila mwaka zaidi ya watu milioni 12 hugunduliwa kuwa na saratani ulimwenguni. Saratani inaua watu wengi zaidi kuliko jumla ya wote wanaokufa na UKIMWI, malaria na kifua kikuu. Lakini ni vizuri kujua ya kuwa kwa kila saratani tano zinazotokea mbili zinaweza kuzuilika na pia ingawaje saratani hazina tiba, nyingi zinaweza kuondolewa kabisa na zisirudi tena.


Mambo yanayochangia kuwepo magonjwa ya saratani

Asilimia 60 ya magonjwa yote ya saratani yanahusishwa zaidi na mtindo wa maisha ambao vipengele vyake ni ulaji, mazoezi ya mwili, matumizi ya pombe na tumbaku. Mambo mengine yanayochangia ni pamoja na virusi na bakteria, madini mazito, mionzi na sumu kadhaa.


Vyakula 

Vyakula huchangia kwa kiasi kikubwa saratani za kinywa na koo, matiti, tezi ya kiume, utumbo mpana, mapafu, tumbo, ini, kongosho na kizazi. Ulaji unaoweza kuchangia ni pamoja na:

Ulaji wa nyama nyekundu kupita kiasi 

Nyama zilizosindikwa 

Vyakula vilivyokuzwa kwa kemikali nyingi (k.m. mbolea), na  Vyakula vyenye mafuta mengi ambavyo huweza kusababisha uzito mwingi 

Vyakula vilivyoota ukungu, kwa mfano karanga.

 

Nyama Nyekundu 

Nyama nyekundu ni muhimu kwa binadamu, lakini ni tatizo inapoliwa zaidi ya nusu kilo kwa wiki. Ulaji wa nyama nyekundu kwa kiasi kikubwa unaongeza uwezekano wa kupata saratani ya utumbo mkubwa. Tafiti zimeonesha ya kuwa kula hadi nusu kilo kwa wiki haiongezi uwezekano wa kupata saratani lakini kila gramu 50 zinazoongezeka huongeza uwezekano wa kupata saratani kwa asilimia 15

 

Nyama Zilizosindikwa

Nyama zilizosindikwa pamoja na zile zilizohifadhiwa kwa kuongezwa chumvi, mafuta, kemikali au kukaushwa kwa moshi (k.m. nyama za kopo, soseji, na bekoni) zinaongeza sana uwezekano wa kupata saratani. Hakuna kiasi chochote cha nyama iliyosindikwa kinachoweza kutumika bila kuongeza uwezekano wa kupata saratani

 

Uzito Uliozidi 

Uzito uliozidi kiasi unamweka mtu kwenye hatari ya kupata magonjwa mengi sugu kwa mfano kisukari, msukumo mkubwa wa damu, magonjwa ya moyo, figo, na saratani za matiti, kongosho na kizazi. Utaratibu mzuri wa kula husaidia kupunguza uzito au kuzuia ongezeko kubwa la mwili.


Pombe na Tumbaku 

Matumizi ya pombe na tumbaku huchangia sana ongezeko la saratani za koo na mapafu. Hapa nchini ongezeko ni kubwa. Asilimia 90 ya wagonjwa waliopokelewa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road walikua na historia ya kutumia vilevi vikali, tumbaku, pilipili kwa wingi na aina nyingine ya vitu vinavyosababisha saratani hii. Pombe inaongeza sana uwezekano wa kupata saratani hasa zile za koo, kinywa, ini na matiti.

 

Virusi na Bakteria 

Saratani za ini, mdomo wa mji wa mimba, mdomo, ngozi, tumbo, mfupa wa taya na kibofu cha mkojo.

 

Vyakula Vinavyopunguza Uwezekano wa Kupata Saratani

Vyakula vitokanavyo na mimea ni kinga nzuri ya kuzuia saratani. Kutumia zaidi vyakula vitokanavyo na mimea husaidia kuondoa uwezekano wa kupata saratani za aina mbalimbali. Inashauriwa kula angalau vipimo vitano vya mboga mbali mbali kila siku. Hakikisha katika kila mlo unatumia nafaka zisizokobolewa sana kama unga wa ngano usiokobolewa sana, unga wa dona, mchele wa brauni, ulezi kwani haukobolewi, na aina mbalimbali za mikunde kama maharage, kunde, choroko, mbaazi, n.k.


Mazoezi ya Mwili

Mazoezi ya mwili yawe sahemu ya maisha kila siku. Inashauriwa kufanya mazoezi ya mwili ya wastani kama vile kutembea haraka haraka angalau dakika 30 kila siku, na mwili ukishazoea ongeza hadi kufikia dakika 60 kila siku. Kama unafanya mazoezi ya nguvu sana basi iwe angalau dakika 30 kila siku. Punguza sana mtindo wa maisha ambao unakufanya uketi bila mazoezi kama vile kuangalia televisheni kwa muda mrefu. Tumia nafasi zote zilizopo za kuzoeza mwili kama vile kupanda ngazi badala ya kutumia lifti, kusaidia kazi za nyumbani, kutembea kwenda sokoni au dukani kama si mwendo mrefu, n.k.


Dalili za Awali za Magonjwa ya Saratani

Magonjwa mengi ya saratani hutibika yakigundulika mapema. Hivyo ni muhimu kumwona mapema mhudumu wa afya kila unapoona dalili zifuatazo:

  • Kukosa hamu ya kula 
  • Kupungua uzito bila sababu 
  • Uchovu bila ya kufanya kazi 
  • Uvimbe wa zaidi ya wiki tatu shingoni, kwapani, tumboni, ngizi au matiti 
  • Kubadilika kwa kawaida yako ya kupata choo (kufunga choo) 
  • Kutokwa na ute, maji maji au usaha ukeni 
  • Kutokwa na damu kwenye choo, mkojo, makohozi au pua 
  • Kwa wanawake, kutokwa na damu ukeni baada ya tendo la ndoa, baada ya kukoma mzunguko wa hethi, au nje ya mzunguko wa hedhi 
  • Shida au maumivi ukimeza chakula au vinyaji 
  • Kukohoa au sauti ya kukwaruza kwa zaidi ya wiki tatu 
  • Matiti kubadilika umbile, uvimbe, ngozi au kutoa maji maji 
  • Kukojoa mara nyingi zaidi ya kawaida yako au mkojo kutoka kwa shida


Aina za Saratani tutakazo zijadili hapa

  1.  TEZI DUME.
  2.  SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI.
  3.  SARATANI YA MATITI
  4.  SARATANI YA NGOZI
  5.  SARATANI YA MAPAFU
read more
Kisukari

Kisukari

Ugonjwa wa kisukari ni hali aambayo inatokea wakati sukari katika damu inakuwa nyingi kupita kiwango cha kawaida kwa muda mrefu. Ili mwili uweze kutumia sukari iliyotoka kwenye vyakula huhitaji kichocheo cha insulini. Insulin husaidia sukari kuingia kwenye chembechembe hai ili kutengeneza nishati-lishe.

Aina za kisukari 

Kuna aina mbili kuu za kisukari ambazo ni;

  1. Kisukari kinachotegemea insulini
  2. Kisukari kisichotegemea insulini

Kisukari kinachotegemea insulini

Kisukari kinachotegemea insulin au “type one diabetes” husababishwa na upungufu au ukosefu wa kichocheo kinachotengenezwa kwenye kongosho kinachoitwa insulini.

Aina hii ya kisukari hudhibitiwa kwa kutumia sindano ya insulin kwani mwili huwa unashindwa kutengeneza kichocheo hiki, pamoja na kurekebisha ulaji. Mala nyingi aina hii ya kisukari huwapata watu wenye umri mdogo (watoto na vijana). Villevile mtu hawezi kurithi iwapo kuna historia ya kisukari katika familia.

Kisukari kisichotegemea insulin

Kisukari kisichotegemea insulin au “type two diabetes” husababishwa na mwili kushindwa kutumia sukari. Mwili wa mtu mwenye aina hii ya sukari huweza kutengeneza insulini ya kutosha lakini haitumiki kuuweesha mwili kutumia sukari na hivyo sukari katika damu huwa katika kiwango cha juu

Aina hii ya kisukari huweza kudhibitiwa kwa kutumia vidonge pamoja na kurekebisha ulaji; au kwa kurekebisha ulaji pekee. Mara nyingi huwapata watu wenye umri mkubwa kuanzia miaka 40 na kuendelea

Kumbuka

  • Ufanisi wa tiba ya aina zote za kisukari hutegemea sana ulaji unaozingatia masharti yatolewayo na mtoa huduma za afya
  • Muonekano wa mgonjwa wa kisukari kinachotegemea insulin mara nyingi huwa ni mwembamba wakati Yule mwenye kisukari kisichotegemea insulin huwa mnene.

 

Mambo yanayoongeza uwezekano wa kupata kisukari

  • Uzito uliozidi (overweight) au unene uliokithiri (obesity)
  • Kutofanya mazoezi
  • Ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi
  • Kuwa na shinikizo kubwa la damu
  • Matumizi ya sigara na bidhaa nyingine za tumbaku
  • Kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40
  • Historia ya kuwa na kisukari katika familia

Dalili za ugonjwa wa kisukari

  • Kukojoa mara kwa mara
  • Kusikia kiu sana
  • Kusikia njaa sana
  • Kuchoka sana na kukosa nguvu bila kufanya kazi
  • Kutoona sawa sawa
  • Kupungua uzito bila kukusudia
  • Kusikia kizunguzungu
  • Kuwa na maambukizi ya ngozi nz vidonda visivyopona upesi
  • Baadhi ya viungo vya mwili kama vidole vya miguu na mikono kufa ganzi

Madhara ya kisukari

Ugonjwa wa kiskari usipodhibitiwa huleta madhara mbalimbali mwilini. Madhara haya huwa makubwa zaidi hasa pale mgonjwa anapokua hazingatii masharti ya matibabu na ulaji bora.

Kuna madhara ya muda mfupi na muda mrefu

Kushuka kwa kiwango cha sukari katika damu

Hali hii hutokea pale ambapo sukari hushuka kuliko kawaida. Hii inaweza kutokana na kutumia dawa kuzidi kipimo, kunywa pombe, kufanya mazoezi bila kula na kutokula kwa muda mrefu.

Dalili za kushuka kwa kiwango cha sukari katika damu

  • Moyo kwenda mbio
  • Mwili kutetemeka
  • Kusikia njaa
  • Kusikia kizunguzungu
  • Kuona mbali (double vision)
  • Kuchanganyikiwa
  • Kutokwa jasho kwa wingi
  • Kuchoka sana

Hali hii ikizidi mgonjwa huweza kupoteza fahamu na hatimaye kupoteza maisha kama hatapata matibabu mapema.

Kama mgonjwa akipatwa na hali hii asipewe kitu chenye sukari, ikiwemo glukosi, soda au juisi.


Kumbuka

 

  • Mgonjwa aliyepoteza fahamu asipewe kinywaji au chakula
  • Anaweza kuwekewa glukosi kidogo kati ya shavu na fizi
  • Awahishwe katika kituo cha huduma za afya haraka iwezekanavyo

 


 

Kupanda kwa kiwango cha sukari katika damu

Hali hii hutokea pale kiwango cha sukari kinapokuwa juu kuliko kawaida. Hii inaweza kutokea wakati mgonjwa anapoacha kutumia dawa, asipotunza dawa vizuri, asipotumia dawa kwa usahihi, anapoacha kufuata masharti ya ulaji unaotakiwa, anapopata maabukizo au maradhi mfano malaria, flu, nimonia nk


Dalili za kupanda kiwango cha sukari katika damu

Kupumua haraka haraka

Kukojoa mara kwa mara hasa wakati wa usiku

Kua na kiu au kukauka koo

Kunywa maji mengi

Kutoona vizur (ukungu)

Kuchoka bila sababu

Miguu na mikono kuchoma

Kizunguzungu

Kuongezeka mapigo ya moyo au moyo kwenda mbio

Kuchanganyikiwa

Kupungukiwa na maji mwilini

Kupoteza fahamu na hatimaye kupoteza maisha kama mgonjwa hatapata matibabu mapema

Kumbuka

Mgonjwa aliyepoteza fahamu asipewe chochote bali awahishwe katika kituo cha kutoa huduma za afya haraka sana                                                                                                                                                 

Madhara ya muda mrefu 

  • Upofu
  • Maradhi ya figo
  • Maradhi ya moyo
  • Vidonda kutopona upesi na hatari ya kukatwa mguu
  • Kufa ganzi na kupoteza hisia za mikono na miguu
  • Kiharusi

Kuzuia kisukari

  • Kula mlo kamili angalau mara tatu kwa siku
  • Epuka kula chakula kingi kupita kiasi
  • Epuka kula chakula chenye mafuta mengi au sukari nyingi
  • Fanya mazoezi ya mwili mara kwa mara
  • Pima sukarikatika damu mara kwa mara, angalau mara moja kwa mwaka
  • Epuka matumizi ya pombe za aina zote
  • Epuka matumizi ya sigara , bidhaa nyingine za tumbaku na madawa ya kulevya.

Jinsi ya kuishi na kisukari

Dhibiti ulaji wako

  • Kula mlo kamili uliotayarishwa kutokana na angalau chakula kimoja kutoka katika kila kundi la vyakula
  • Kula vyakula vya nafaka kama ulezi, mtama, uwele, ma nafaka zisizokoboewa kwa mfano dona, ngano, au shairi
  • Kula mboga mboga kwa wingi kwa mfano mchicha, matembele, karoti, majani ya maboga, kisamvu, mlenda nk
  • Kula kiasi kidogo cha vyakula vya nafaka, mizizi na ndizi katika mlo
  • Kula vyakula vya jamii ya kunde kama mboga (sehemu ya mlo) kwa mfano maharagwe, njegere, mbaazi, kunde, choroko, nk
  • Kula matunda kwa kiasi mfano ndizi au chungwa moja au kipande cha papai au embe kubwa katika kila mlo
  • Kunywa maji kwa wingi
  • Epuka ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi kama jamu, asali, chokoleti, pipi, bazooka, aiskrimu, na juisi bandia
  • Epuka ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi
  • Epuka unywaji wa pombe

Fanya mazoezi mara angalau nusu saa kwa siku

Tunza miguu yako kwa makini

  • Epuka kuvaa viatu au soksi zinazo bana
  • Epuka kuvaa viatu vyenye kisigino kirefu ambacho huweza kusababisha kuanguka na kuumia
  • Osha miguu yako kwa maji safi na kausha vizuri hususan katikati ya vidole
  • Usitembee bila kuvaa viatu
  • Vaa viatu vya wazi na vyenye kisigino kifupi
  • Epuka kijiumiza, na unapokua na kidondatibu mapema

Epuka msongo wa mawazo zingatia

  • Afya ya kinywa kwa kupiga mswakiangalau mara mbili kwa siku
  • Usafi wa mwili
  • Taarifa a elimu kuhusu kisukari
  • Taarifa na elimu kuhusu kisukari
  • Masharti ya dawa na ulaji
  • Kuhudhulia kliniki kama inavyoshauriwa
  • Kumuona daktari mapema mara unapopata tatizo lolote la kiafya


Angalizo

  • Awe makini na ulaji wake, hussani akiwa shuleni
  • Azingatie na aoanishe muda wa kupata sindano ya insulin na muda wa kula
  • Asaidiwe kuepuka kula vyakula visivyo bora kilishe
  • Afikiriwe na aangaliwe wakati wa michezo, mazoezi, na kazi za kutumia nguvu
  • Waalimu washirikiane n wazazi au walezi kuhakikisha motto anapata asusa zenye virutubishi muhimu anapokua shuleni
read more
Shinikizo kubwa la damu

Moyo unapopiga, husukuma damu kwenye mishipa ya damu ili isambae mwilini kote. Shinikizo la damu ni hali ambapo msukumo huu wa damu unazidi kiwango cha kawaida na unaweza kusababisha madhara mwilini. 


Shinikizo kubwa la damu

Visababishi vya shinikizo kubwa la damu 

Sababu zinazochangia mtu kupata shinikizo kubwa la damu ni pamoja na:- 

  • Matumizi ya chumvi kupita kiasi hasa ya kuongeza mezani. 
  • Utumiaji wa pombe kupita kiasi. 
  • Utumiaji wa tumbaku na bidhaa zake.
  • Msongo wa mawazo kutokana na vitu kama vile majanga, unyanyasaji wa kijinsia, n.k. 
  • Umri mkubwa (Miaka 60 na kuendelea). 
  • Historia ya shinikizo kubwa la damu katika familia. 
  • Uzito mkubwa kupita kiasi - kumbuka unene hauashirii hali nzuri ya maisha bali ni ugonjwa.  Kutokufanya mazoezi ya mwili. 
  • Ugonjwa wa kisukari.


Dalili za shinikizo kubwa la damu 

Wengi wa watu wenye shinikizo kubwa la damu hawana dalili zozote. Waliobaki wanaweza kuwa na dalili zifuatazo:

  • Kuumwa kichwa mara kwa mara.
  • Kutoona vizuri.
  • Kizunguzungu. 
  • Moyo kupiga kwa nguvu au haraka haraka  Kutokwa na damu puani. 
  • Maumivi ya kifua au kupumua kwa shida.
  • Uchovu wa mara kwa mara. 

Ili kugundua kama una shinikizo kubwa la damu ni vyema kupima msukumo wa damu kila unapoenda kwenye kituo cha tiba au kupima angalau mara moja kwa mwaka. 

Wakati mwingine, watu wenye shinikizo kubwa la damu gafla wanaweza kuwa na dalili za kiharusi kama ilivyoelezwa ukurasa unaofuata. 

Ni vyema ukiona dalili hizi usisite kutafuta msaada wa mhudumu wa afya.

 

Madhara ya shinikizo kubwa la damu 

Shinikizo kubwa la damu linaweza kuleta madhara mbalimbali yakiwemo:

  • Kupasuka kwa mishipa ya damu kichwani na kusababisha kuharusi.

Kiharusi ni moja ya sababu kubwa za vifo vya watu wazima 

  • Moyo kupanuka na hatimaye kushindwa kufanya kazi yake ya kusukuma damu. 
  • Kuharibika kwa mishipa ya damu kwenye figo na hatimaye figo kushindwa kufanya kazi yake ya kusafisha damu. 
  • Mishipa mikubwa ya damu kuharibika kwa sababu ya kuvuja kwa virutubishi vilivyo kwenye damu na kusababisha kiharusi, ugonjwa wa moyo au miguu kutopata damu ya kutosha. 

 

Kuzuia shinikizo kubwa la damu 

Shinikizo kubwa la damu linaweza kuzuilika kwa kuzingatia yafuatayo: 

  • Punguza matumizi ya chumvi:

chumvi isizidi kijiko kidogo cha chai kwa mtu mmoja kwa siku (angalia sura ya ulaji unaofaa).

  • Epuka kunywa pombe kupita kiasi (angalia sura ya pombe). 
  • Fanya mazoezi ya viungo mara kwa mara na kujishughulisha na kazi mbalimbali mradi mwili upate mazoezi ya angalau nusu saa kila siku (angalia sura ya mazoezi). 
  • Epuka uzito mkubwa kupita kiasi na unene (angalia sura ya unene). 
  • Epuka matumizi ya tumbaku na bidhaa zake (angalia sura ya tumbaku).
  • Kula matunda na mboga mboga kila siku (angalia sura ya ulaji unaofaa)
  • Punguza msongo wa mawazo (angalia sura ya msongo wa mawazo).
read more
Magonjwa ya moyo

Magonjwa ya moyo

Moja wapo ya sababu za magonjwa ya moyo ni kuziba kwa mishipa ya damu inayosambaza damu kwenye misuli ya moyo. Kuziba kunaweza kusababishwa na mafuta yanayotokana na chakula kinacholiwa. Mafuta haya huganda katika kuta za mishipa hiyo, hali ambayo hutokea pole pole na huchukua muda mrefu hadi mishipa kuziba kabisa. Shinikizo la damu, tumbaku, uzito uliozidi na kutofanya mazoezi huchangia sana uharibuvu huu.

  • Dalili za magonjwa ya moyo

Kadiri mishipa ilivyoziba, misuli ya moyo hukosa oksijeni na virutubishi hali ambayo inasababisha dalili zifuatazo:

  • Maumivu ya kifua ambayo hutokea zaidi mtu anapojitahidi kujishughulisha na kutoweka anapopumzika
  • Moyo kwenda haraka 
  • Uchovu na kukosa nguvu ya kufanya kazi 
  • Ikiwa sehemu kubwa ya moyo imeathirika, moyo hushindwa kabisa kufanya kazi.



Kuzuia magonjwa ya moyo

  • Hakikisha uzitowako uko katika kiwangokinachofaa kwa kufuata ulaji na mtindo bora wa maisha 
  • Chagua vyakula vyenye mafuta kidogo kama vile matunda, mbogamboga, nafaka zisizokobolewa. 
  • Chagua nyama na maziwa yasiyo na mafuta mengi. 
  • Epuka vyakula vyenye sukari nyingi na mafuta mengi kama siagi, keki, chokoleti; na vyakula vilivyokaangwa kama chipsi, kuku, na maandazi, sambusa na vitumbua
  • Lehemu ni aina maalum ya mafuta ambayo mara nyingi hupatikana katika maini, sehemu ya njano ya yai, siagi, barafu, na nyama yenye mafuta mengi. Aina hii ya mafuta huongeza sana uwezekano wa kuziba mishipa ya damu hivyo epuka kula vyakula hivi vyenye lehemu nyingi. 
  • Inashauriwa kufanya mazoezi ya mwili kwa dakika 30 hadi 60 kila siku.  Epuka kukaa bila kufanya shughuli yoyote. 
  • Epuka uvutaji wa sigara na matumizi ya tumbaku ambavyo huchangia katika kuleta magonjwa ya moyo 
  • Epuka unywaji wa pombe kwani unachangia kwenye kuongeza uzito na huingilia matumizi mazuri ya chakula mwilini

Aina za magonjwa ya moyo

Matibabu ya magonjwa ya moyo

Kiharusi

read more